<?xml version="1.0" encoding="UTF-8"?><song><hymn_number>69</hymn_number>
<title>Twendeni Askari TZR69</title>
<lyrics>[V1]
 Twendeni askari, watu wa Mungu;
 Yesu yuko mbele, tumwandame juu.
 Ametangulia Bwana vitani,
 Twende mbele kwani ndiye amini.

[V2]
 Twende askari watu wa Mungu;
 Yesu yuko Mbele, tumwandame juu.

[V3]
 Jeshi la Shetani, likisikia
 Jina la Mwokozi, litakimbia,
 Kelele za shangwe zivume nchi;
 Ndugu inueni zenu sauti.

[V4]
 Kweli kundi dogo, watu wa Mungu
 Sisi na mababa tu moja fungu.
 Hatutengwi nao, moja imani,
 Tumaini moja, na moja dini.

[V5]
 Haya mbele watu nasi njiani,
 Inueni myoyo, nanyi sifuni;
 Heshima na sifa ni ya Mfalme,
 Juu hata chini, sana zivume.</lyrics>
</song>